BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Masomo matano (05) utakayojifunza kutoka kwenye kitabu cha Never Eat Alone cha Keith Ferrazzi.

 


Hapa kuna masomo matano kutoka kitabu cha "Never Eat Alone, Expanded and Updated: And the Other Secrets to Success, One Relationship at a Time" kilichoandikwa na Keith Ferrazzi:

1. Uwezo wa kujenga mtandao:  kila wakati kuwa na uwezo wa kujenga mtandao wenye thamani maishani mwako. Mtandao huu ni ule wenye uwezo wa kufahamiana na watu mbalimbali ambao watakusaidia sana kuweza kufungua milango ya fursa, misaada mbalimbali na ushirikiano mzuri wa kiutendaji kwenye vitu vyenye tija vitakavyokusaidia kuweza kutimiza malengo yako.

2. Kuwa mkarimu na  mkweli: unapaswa kuwa mkarimu na mkweli kwa watu wengine. Epuka kuwa na tabia ya uongo kwa watu wengine hii itakujenga dhana ambayo watu wengine watakuwa hawakuamini hivyo watu hao watajitenga nawe. Pia jenga dhana ya kuwasaidia watu wengine kuliko kutegemea watu wengine kwenye kila jambo, kwa maneno mengine jifunze kurudisha fadhila kwa watu wengine ili kuimarisha mahusiano yenu.

3. Jenga  mahusiano yenye ufanisi: mwandishi wa kitabu hiki anasisitiza sana suala la kujenga mahusiano yenye ufanisi, ambapo unatutaka tuwe ni watu wenye kuwasikiliza watu wengine, kuonyesha nia ya dhati kwa wengine pale wanapotuhitaji lakini pia mwandishi anatuhimiza kuendelea mahusiano tuliyoyatengeneza yawe ni ya muda mrefu ili tuweze kufanikiwa zaidi na zaidi.

4. Tengeneza hali ya ushindi kwa wengine: Mwandiahi anaweka msisitizo kuwa kila wajati tafuta njia za kusaidia wengine kuweza kufikia malengo yao na kutatua matatizo yao yanayowakabili, huku ukiwa  unafahamu kwamba mafanikio ya pamoja yanazalisha mahusiano yenye nguvu kila wakati. Epuka kuwa ni mtu mbinafsi bali kuwa tayari kuruka pamoja na wengine ila kuweza kukua kwa pamoja.

5. Jenga shukrani kwa watu wengine pia: Kila wakati jifunze kuonesha shukrani kwa watu ambao wamekuwa wakikusaidia kwenye mambo mbalimbali. Lakini pia endelea kuwasilina na watu hao mara kwa mara ili mahusiano yenu yawe ni mahusiano yenye uimara kila wakati. Pia tekeleza kile ulichokiahidi kupitia kwa watu hao huku ukiendeleza juhudi ya ushirikishi wa mambo yenu ili kuendeleza mahusiano yaliyo na maana.

Kitabu hiki ni muongozo mzuri wa kukupa matokeo uyakayo kwenye kila jambo unalolifanya endapo utajenga na kudumisha mahusiano mazuri ambayo umejenga na watu wengine.

Tukutane kwenye uchambuzi mwingine siku ya jumapili ijayo!

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments