BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha "How to Raise Your Own Salary" cha Napoleon Hill.


Hapa kuna mafundisho saba muhimu kutoka kitabu cha "How to Raise Your Own Salary" kilichoandikwa na Napoleon Hill.

1. Tambua kusudio maalum: kila mtu ameumbwa na kusudio lake, kila mtu anapaswa kuliishi kusudio hilo. Kwenye hili unatakiwa kujua lengo au kusudio lako la maisha, ukishalijua kusudio lako unapaswa kujitoa kikamilifu kwenye jambo hilo huku ukiweka jitihada zako ili uweze kukamilisha lengo lako. 

2. Jifunze sanaa ya kujidhibiti: Kama hutokuwa mtu wa kujidhibiti basi fahamu kuwa kila kitu kitakuwa ni kichungu sana kwako. Mwandishi anatutaka tuwe ni wa watu kujidhibiti sana ili tuweze kufanikiwa.
Kujidhibiti ni muhimu kwa mafanikio hata katika jambo lolote lile. Kwenye hili Napoel Hill anasisitiza umuhimu wa kujenga tabia za kujidhibiti kupitia mazoea kama vile usimamizi wa muda, kuweka malengo, na ujifunzaji endelevu. Kwa kudhibiti fikra, hisia, na vitendo vyako, unaweza kushinda vikwazo na kufikia malengo yako.

Thibiti yale mambo yote yanayokukwamisha kufanikiwa, anza mara kujenga mambo chanya yatakayokufanikisha kwenye kila ulifanyalo.

3. Jenga mtazamo chanya: mwandishi Napoleon Hill anasistiza suala la kutaka watu wajenge imani kuwa kila kitu kinawezekana na huo ndiyo mtazamo chanya. Pia mwandishi anasema mtu anapojenga mtazamo chanya anajenga uwezo wa kutatua pia kila changamoto inayojitokeza kwenye kila harakati zako uzifanyazo. Mtazamo chanya ni chachu ya kila fanikio lako, hivyo kila wakati kuwa mtu wa mtazamo chanya.

4. Chukua hatua: Mafanikio mara nyingi yanahitaji kuchukua hatua. Mafaniko hayaendi kwa mtu aliyetulia tu bali mafaniko huenda kwa mtu ambaye anachukua hatua. Hatua za kiutendeji ndizo zitakazokupa mafanikio. 

Tengeneza fursa zako mwenyewe kwa kuchukua hatua za kiutendaji, haijalishi ni vikwazo gani utakavyokutana navyo bali hakikisha kuwa unakuwa mtu wa kuchukua hatua za kiutendaji.

5. Endeleza ujuzi wa mawasiliano: ujuzi wa mawasiliano mara nyingi huusisha mambo makubwa yafuatayo, kwanza ni kusikiliza kwa umakini, kuhamasisha wengine, kujenga uhusiano mzuri na watu wengine na mwisho kufanya majadiliano kwa ufanisi na watu wengine. Ukifanikiwa kuyajenga hayo kwa ubora itakuwa ni rahisi zaidi kwako kuwa bora kwenye maisha yako.

6. Usigope changamoto: Mafanikio mara chache yanakuja bila vikwazo na vizuizi njiani. Hill anawafundisha wasomaji kujenga uvumilivu na uthabiti, kutokukata tamaa mbele ya changamoto.  Kuendelea kupambana bila kuchoka kwenye kila changamoto hatimaye kupata mafanikio tuyatakayo.

7. Tafuta kuwa bora daima: Ukuaji na maendeleo ya kibinafsi ni mchakato endelevu unaohitaji kujitoa zaidi na kuwa na juhudi.  Mwandishi anahimiza suala la kujifunza kila wakati, kwani kila ajifunzaye anagundua fursa mpya kila siku. Endelea kujifunza kila wakati kwa sababu unajenga uwezo wako binafsi wa kitaaluma.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments