Kufanikiwa au kushindwa sio matokeo ya kuamka leo umefanikiwa au kuamka leo umeshindwa. Kwa lugha nyingine kufanikiwa au kushindwa ni matokeo ya maamuzi madogo madogo unayoyachukua kila siku, ndiyo yanakufanya ufanikiwe au ushindwe kwenye maisha yako.
Kila wakati kuwa makini sana na maamuzi unayoyafanya kila siku. Kwa maamuzi hayo ndiyo yanayokufanya ufanikiwe au ushindwe. Jaribu kuangalia pale uliposhindwa yote hiyo ilisababishwa na maamuzi ya aina fulani na pale uliposhinda pia yote hiyo ilitokana na maamuzi ya aina fulani uliyoyafanya.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
0 Comments