Kama watu wote wanaokuzunguka wapo tu na hawajali kitu,...inatakiwa uwe mtu wa tofauti, wewe jali.
Kama watu wanaokuzunguka wamejaa na hofu na wasiwasi mwingi,... inatakiwa uwe tofauti jaa ujasiri na kujiamini.
Kama watu wanaokuzunguka ni wavivu wa kupindukia,... unatakiwa uwe mtu wa tofauti na uweke juhudi kubwa.
Kama watu wanaokuzunguka hawafanyi kazi kwa ubora,...unatakiwa uwe wa tofauti na ufanye kazi zako kwa ubora.
Kwa vyovyote vile jamii inayokuzunguka ilivyo, acha kufuata mkumbo, ishi kwa viwango vya ubora wako.
Wakati wote unatakiwa ufanye yaliyo bora, uishi kwa ubora bila kujali wale wanaokuzunguka wanaishi vipi maisha yao.
Kwa kuishi maisha ya ubora, hapo ndipo utamudu kujenga msingi mkubwa wa mafanikio yako. Anza sasa, usichelewe.
Imeandikwa na Benson Chonya!
0 Comments