BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kufanya kila siku.



Yapo majukumu ambayo kila siku ni lazima uyatekeleze. Jambo zuri la kufanya ili majukumu hayo uyatekeleze vizuri, anza na majukumu ambayo kwako unayaona ni magumu na ya muhimu.

Unapoanza na majukumu magumu na muhimu sana kwako, hiyo inakupa urahisi kwa majukumu mengine kuyafanya, kwani kwako itakuwa ni rahisi, kwa sababu yale majukumu yakuumiza kichwa unakuwa huna tena.

Kitu cha kufanya kila siku, hakikisha, unaanza na majukumu magumu kwako na muhimu kabla akili haijachoka. Akili ikishachoka, anza kutekeleza majukumu mepesi mepesi, utashangaa  na majukumu mengine unayamaliza kirahisi tu, kwa sababu hayatumii akili na nguvu nyingi.

Na; Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments