Kuna ukweli ambao huwezi kuukwepa ya kwamba, ubora wa maisha yako, unakutegemea wewe. Ubora wa maisha yako huwezi kuazima, au huwezi kuutoa kutoka kwa boss wako, serikali au ndugu yako, ubora huo unakutegemea wewe.
Mawazo uliyonayo na hatua unazochukua ndizo zinazofanya maisha yako yawe bora. Huwezi kupita njia ya mkato ya maisha yako. Unalazimika kuishi kwa nidhamu, na kukubali kukutana na changamoto.
Ili kufanya maisha yako bora, unatakiwa ujue kila siku inakuja na fursa, lakini fursa hizo zinakuja zikiwa katika mfumo wa changamoto. Ni jukumu lako kutumia mawazo na kuchukua hatua kuzipata fursa hizo na kufanikiwa.
Kila siku kwa sababu inakuwa ni siku ya fursa, unatakiwa utumie juhudi, kujitoa, na kuweka nguvu za uzingativu ili uweze kuwa bora kwenye maisha yako.
Kwenye maisha yako unao uchaguzi, kuishi kujisimamia na kuishi maisha yenye MALENGO na MAANA, au kukaa na kulala na uwaangalia wengine wanavyofanya maisha yao.
0 Comments