Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata bila changamoto. Kama unafikiri mafanikio ya namna hiyo yapo, basi ujue unajidanganya.
Kila wakati inabidi utambue changamoto ni kitu cha kawaida katika safari ya mafanikio. Hautaweza kukwepa changamoto kama unataka kufanikiwa.
Kila wakati wakati unapokutana na changamoto zinakusaidia kukufanya kuwa imara na kujenga msingi kamili wa mafanikio.
Acha kulia na kulalamika sana kila unapokutana na changamoto. Jifunze kujua namna ya kutumia changamoto kukusaidia kufanikiwa zaidi.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.
0 Comments