BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo saba (07) ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha Win Your Inner Battles cha Darius Foroux.


Leo tuangalie japo kwa achache yale yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Win Your Inner Battles kiliandikwa na Darius Foroux. 

Nimekuletea mafundisho mazito saba kutoka kwenye kitabu "Win Your Inner Battles":

1. Kila mmoja wetu anapaswa kutambua maadui zake wa ndani. Kitabu kinadai kwamba vizuizi vikubwa zaidi mara nyingi hujificha ndani yetu, katika mfumo wa mawazo hasi, shaka juu ya sisi wenyewe, hofu, na kuahirisha. Kwa nukta hiyo kumbe maadui kama vile wasiwasi, hofu na mawazo hasi yamekuwa ni jambo tata sana kwetu. Tunapaswa kuwajua maadui hao wa ndani ili kushindana nao na hatimaye kushinda.

2. Jenga ufahamu wa ndani. Kila mmoja ana unfahamu wa ndani hivyo yatupasa kuuendeleza ufahamu wa ndani ili kutambua vita vyako vya ndani.  Kaa chini kisha tafakari kuhusu ufahamu wako wa ndani, angalia mambo yale ya msingi ambayo ni chanya katika mawazo yako kisha chukua daftari na kuyaandika mambo hayo.

Mambo hayo kama yana tija kwako ni muhinu uanze mara moja kuyatekeleza. Unapoandika ufahamu wako wa ndani unaweza kupata uelewa wa kina wa mawazo yako, hisia, na motisha zako zenye kukupeleka nchi ya asali na maziwa.

3. Chuguza kuhusu vita vyako vya ndani, uhalisia ni kuwa kuna vita vizuri na vita vibaya vilivyomo ndani yako,  Si vita vyote vya ndani vinavyostahili kupigwa. Jifunze kutofautisha kati ya vile vinavyokuzuia kufanikiwa na vile vitakavyokusaidia kufanikiwa. 

Tumia nguvu yako kushughulikia vita vinavyothamini maendeleo yako na ustawi wako. Yachukulie kwa uzito kila mawazo mazuri ili uweze kuwa bora, na yapinge vikali mawazo mabaya ambayo si msaada wala lolote kwako.

4. Badilisha mawazo hasi na kauli mbaya zinazojitengeneza ndani yetu. Mazungumzo yetu ya ndani yanacheza jukumu kubwa katika kuunda ukweli wetu. Kitabu kinahimiza zaidi kubadilisha mazungumzo hasi ya ndani na kauli hasi ambazo mara nyingi huwa tunazifikiri na kutukatisha tamaa. Mwandishi anataka tuwe ni watu wa kujinenea yaliyo mema kila wakati na kutafuta kauli hamasishi zenye kututia moyo. 

5. Chukua hatua mara moja. Kushinda vita vya ndani kunahitaji zaidi kuchukua hatua za kiutendaji. Kama kuna sauti ndani inakuambia mawazo chanya, basi usiishie kuwaza bali anza kutenda mara moja yale uyawazayo. Pia Kitabu kinaeleza umuhimu wa kuchukua hatua na kujenga kasi kuelekea malengo yako. Hata hatua ndogo zinaweza kusaidia kuvunja mifumo ya kujizuia na kusonga mbele.

6. Lijue kusudi na shauku yako. Kugundua kusudi lako katika maisha kunaweza kutoa silaha yenye nguvu dhidi ya mawazo hasi yaliyo ndani yako. Unapoijua shauku shako imani yako kubwa itakuwa inakuambia kuwa kila jambo linawezekana. Unapokuwa na maono wazi ya kile unachotaka kufanikisha, utaondokana na hofu pia, hivyo utaondokana na wasiwasi pia.

7. Unapokosea kubali kuanza upya. Kwa kuwa wewe ndiyo mtalawa wa maisha yako, inapotokea umekosea basi ni vyema ukakubali kuwa umekosea na iruhusu nafsi yako kuanza upya. Unapokosea unapata wasaa mzuri kujifunza jambo vizuri ambapo kama utarekebisha makosa yatakusaidia kwenda mbele.

Kwa leo naomba tuishie hapo tukutane kwenye kitabu kingine.

Ndimi afisa mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments