BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze haya kutoka kwenye kitabu cha Miracle Morning, The Six Habit That Will Transform Your Life Before 8am.

Jifunze haya kutoka kwenye kitabu cha Miracle Morning, The Six Habit That Will Transform Your Life Before 8am.

Kitabu cha The miracle Morning, The six habit that will transform  your life before 8AM kilichaondikwa na Hal Elrod ni miongoni mwa vitabu ambavyo vinazungumzia miujiza ambayo itayabadili maisha yako endapo utafanya mambo msingi kabla saa mbili kamili asubuhi.

Mwandishi Hal Elrod alianzisha dhana uliyofamika kwa  la SAVERS routine ikiwa inakilisha mambo yafuatayo;

S- Silince (utulivu)

A- Affirimations (kuthibitisha)

V- Visualization (Taswira)

E- Exericises (Mazoezi)

R- Reading (kusoma)

S-Scribing (kuandika)

S- Silince (utulivu) kupitia dhana hiyo ya SAVER mwandishi anazungumzia S ya kwanza akitutaka sana tuwe na watu wenye utulivu zaidi wa kimawazo hasa nyakati za asubuhi. Utulivu huo ni ule wa kiakili zaidi kabla mambo hayajaanza kuwa mengi. Unapokuwa na utulivu inakupa nguvu ya kutafakari mambo muhimu chanya katika maisha yako. 

A- Affirimations (kuthibitisha) kupitia dhana hiyo ya SAVER mwandishi anazungumizia herufi A ambapo anatuasa tuwe na tabia ya kujinenea hasa yale yaliyo chanya kila siku asubuhi, unapojinenea yaliyo chanya inakupa nguvu yakuyatenda yale yaliyo jinenea, unapofanya hivyo basi yale uliyojinenea unayathibitisha kwa kuwa yaweka katika matendo hasa pale siku yako inapooanza.

V- Visualization (taswira) kupitia dhana hiyo hiyo ya SAVER mwandushi anaizungumzia herufi V ikiwakilisha visualization ambapo kwa kishwahili ni taswira. Visualization ni ile picha ambayo mtu huijenga kichwani mwake kabla jambo husika halijawa katika uhalisia. Hivyo mwandishi anasema kabla hujaanza  siku yako ni lazima uwe na picha kamili ya kile ukitakacho. Pia kwenye hili lazima upange ratiba asubuhi ya mambo unayopaswa kuyafanya kabla ya kuianza siku yako.

E- Exericises (mazoezi) kupitia dhana hii mwandishi anasema kila wakati tunapaswa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi, mazoezi haya yanapaswa kuwa angalau ni ya dakika chache ili mwili uwe vizuri. Mazoezi ni afya husaidia sana kumpa mtu nguvu ya kiutendaji wa kazi zake kwa siku husika.

R- Reading (kusoma) mwandishi anatuasa sana tuwe na utaratibu wa kusoma mambo muhimu yahusuyo masuala ya kimaendeleo binafsi. Asubuhi ni muda ambao bado ni tulivu sana kwako, hivyo weka wa kusoma walau mambo machache yatakayokupa fikra chanya.

S- Scribing (kuandika) weka utaratibu wa kiandika mipango na mambo muhimu. Andika yale uliyoyasoma, andika mambo muhimu unayokwenda kuyafanya. Ipo nguvu nguvu kubwa sana ya kuandika. Unapooandika inakukumbusha nini unatakiwa kufanya.

Kitabu cha hiki cha The miracle morning kimekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha ya wengi hasa wale walioitumia kanuni hiyo SAVERS. Litakuwa ni jambo jema zaidi kwako endapo hata wewe utaamua kutumia kanuni hizo kama unaataka miujiza ya kimafanikio.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments