BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Aina hii ya hofu imewapoteza wengi sana.

Wapo baadhi ya watu wanashindwa kufanya vizuri katika jambo fulani kwa sababu watu hao wanasongwa na hofu ya kupoteza kitu fulani. Watu wengi wanaogopa kuanzisha biashara fualani kwa sababu watu hao  wanaogopa kupoteza fedha zao katika biashara fulani kwani wanaona hawatapata faida.

Aina hii ya hofu imekuwa ikiwasonga wengi mwanzoni kabisa kabla ya kuanzisha jambo fulani.  Aina hii ya hofu imeua ndoto za wengi sana na kusababisha watu hao kufa ni vitu vikubwa sana ambavyo vilipaswa kuanzishwa ila kutokana na hofu hiyo watu hao wameshindwa  kuvifanya.

Hivyo ili kuweza kuishinda aina hii ya hofu ya kuhofia kupoteza jambo fulani basi ni muhimu kuweza kufanya uchunguzi yakinifu kabla ya kuamua kuanzisha jambo fulani, lakini pia kumbuka namna pekee itakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kushinda aina hii ya hofu unatakiwa kuelewa hakuna mafanikio yasiyo ya changamoto hivyo unatakiwa kujiamini, kama umeamua kufanya jambo fulani wewe fanya epuka na aina hiyo ya hofu kwani ni kikwazo kikubwa cha ndoto za watu wengi sana.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments