Inaaminika ya kwamba mtu akifanya vizuri katika jambo fulani basi mtu huyo anatakiwa kupewa zawadi, mtu huyo hupewa zawadi ili kuonesha pongezi kwamba watu wengine wanatambua mchango wake kwenye kile akifanyacho. Pia wakati mwingine zawadi hongeza hamasa kwa mpokeaji wa zawadi hiyo kwamba aongeze juhudi za kufanya vizuri zaidi.
Kama ilivyo utaratibu huo wa kumpa zawadi mtu mwingine, basi hata wewe unatakiwa kuanzisha utaratibu wa kujipa zawadi hasa pale ufanyapo vizuri kwenye jambo fulani.
Kwa mfano mimi binafsi nikikamilisha jambo fulani kwa wakati huwa ninao utaratibu wa kujipongeza wa kujipa zawadi kwa kujitoa “out” pamoja na kula chakula nikipendacho, huo ni utaratibu wangu na wewe unaweza kuanzisha utaraibu wako kadri utakavyoona inafaa.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments