Mara nyingi sana, hakuna mtu ambaye anapenda kufatilia vitu vilivyokufa au vitu vilivyokosa matumaini. Kila mtu anapenda kufatilia vitu vilivyo hai, vitu ambavyo vinaweza vikamsaidia leo na kesho pia.
Kwa mfano, kama umelima shamba, na shambani kwako kuna mimea imekufa, mimea hiyo iliyokufa utakuwa huna muda wa kuifatilia kabisa, utachokuwa ukifatilia ni mimea hai na yenye faida kwako.
Na kwenye maisha iko hivyo hivyo. Hakuna mtu ambae yuko tayari kufatilia vitu vilivyokufa. Ukiona watu hawakufatilii sana, basi elewa mambo yako mengi yamekufa na hakuna wa kutaka tena kuyajua.
Kama mambo yako mengi yamekufa, hakuna wa kukufatilia hiyo iko wazi. Kama unataka mambo yako yaanze kufatiliwa hakikisha kila kitu unakifanya kiwe hai. Kila kitu kifufue, utafatiliwa sana na hutaamini.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments