Uvumilivu ndiyo nguzo kubwa kwa anayesaka mafanikio. Uvumilivu ni muhimu kwa sababu hata wahenga walinena kwamba “mvumilivu hula mbivu” na kila avumiliaye atafanikiwa, hiyo ni yangu nimeongoza ila ndiyo ukweli halisi, kwamba kama kweli unataka kufikia kilele cha mafanikio yako basi unapaswa kuwa mvulivu.
Unapaswa kuvumilia kwenye kila ulifanyalo kwa sababu si kila jambo ambalo utalifanya leo litaleta matokeo chanya leo leo, hapana matokeo mengine huwa yanachelewa sana kuonekana hivyo unatakiwa kuwa mvulivu huku ukiongoza juhudi na jitihada kwenye hatua zako za utendaji wako wa kazi.
Ni muhimu kuwa mvulimivu kwa sababu wengi wa watu wengi wamekuwa wakitaka kufanikiwa katika mambo yao kwa kutumia njia za mkato, kitu hicho kimawapelekea watu hao kutokudumu katika mafanikio hayo, Naomba usiwe ni mmoja wapo.
Ninachokuasa ni kile kile kwamba unapaswa kuwa mvumilivu kwenye kila kazi ambayo unayofanya huku ukiongeza juhudi zako binafsi za kiutendaji zitakazokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kufikia kilele cha mafanikio yako, epukana na uharaka wa kufanikiwa kwani hutoweza kufikia lengo na hata kama utafikia lengo basi hutoweza kudumu katika mafanikio hayo.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments