BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kujifunza kutoka kwenye Do The Work kilichoandikwa na Steven Pressfield



Kitabu "Do the Work" kilichoandikwa na Steven Pressfield kinatoa mwongozo mzuri wa kufanya kazi na kufanikisha malengo. Kitabu hiki kitakupa muongozo maridhiwa wa kiutendaji wa kazi zako ili upate matokeo sahihi.

Kitabu cha Do the work ni kinachokuongeze hamasa za kiutendaji wa kazi zako, hasa pale unapokuwa umekata tamaa au pale unapokuwa huoni matokeo tarajiwa ya yale uyafanyayo.

Yafuatayo ni baadhi utakayojifunza kutoka kwenye kitabu hiki cha " Do The Work" 

Kuanza ni muhimu
Unapotaka mabadiliko makubwa katika maisha yanzo usiwe mtu wa polojo polojo bali unatakiwa kuanza kutenda. Kutenda ni hatua ya kwanza muhimu katika kufanya kazi yoyote.

Unachopaswa kuelewa ni kwamba ili uone matokeo, acha stori bali chukua hatua za kuanza kufanya jambo hilo, unapochukua hatua ni kwamba utaanza kupata matokeo ya kazi ambayo utakuwa umeanza kufanya.

Kushinda uoga.
Uoga ni adui mkubwa sana wa mafanikio ya wengi, unapotaka kushinda kwenye jambo lolote unapaswa kuweka hofu yako kando kwani kushinda hofu na wasiwasi ni muhimu ili kuanza na kudumisha mchakato wa kufanya kazi utakaokupa matokeo sahihi. 

Shinda hofu ili uweze kuwa bora zaidi katika maisha yako.

Kujitoa kwa moyo wako wote.
Epuka kufanya jambo lolote kwa kujaribu, bali unapaswa kujitoa kwa moyo wako wote katika kufanya jambo hilo. Unapojitoa moyo na akili zako zote zinakuwa sehemu hiyo. Unapaswa Kujitoa kikamilifu kwa kile unachokifanya ni msingi wa mafanikio yako, yakupasa ujitoe ili upate matokeo sahihi.

Kuvumilia changamoto.
Kwenye kila kazi yeyote ile kuna changamoto ndani yake, hivyo huna budi kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto zozote ambazo zinajitokeza pindi utafutapo majibu sahihi ya changamoto husika.

Kujifunza kutoka kwa kila uzoefu.
Maisha ni kujifunza, usiache kujifunza, kwani kila jaribio linaweza kufundisha somo muhimu ambalo litakusaidia kupigia hatua fulani kwenye kazi yako. Endelea kujifunza kwa sababu kujifunza ni shule itakayokusaidia kupata matokeo chanya zaidi.

Kuwa na fikra chanya
Kwenye kazi yeyote ile uifanyayo unapaswa kujifunza kuwa na fikra chanya, mtu akiwa na fikra chanya humsaidia mtu huyo kuwa chanya pia. Unapokuwa na fikra au mtazamo chanya kunaweza kusaidia kukabiliana na vikwazo na changamoto.

Kufanya kazi kwa muda mrefu.
Kufanikiwa kunahitaji kujitoa kwenye kazi yako kwa muda mrefu badala ya kuzingatia matokeo ya haraka. Unapofanya kazi kwa muda mrefu yapo mambo ambayo utajifunza kupitia kazi hiyo, mosi unapata uzoefu wa kutosha, lakini pili unakuwa ni mbobezi wa kukabiliana na changamoto zinazojitokea kwenye kazi hiyo.

Kuwa na nia thabiti.
Kitabu hiki kinatutaka kuwa na nia thabiti. Nina thabiti ni ule uwezo wa Kuwa na lengo lililowazi na kufanya kazi, ukiwa na lengo wazi itakusaidia sana kufanya kazi zako  bila kukata tamaa. Hivyo kila wakati unapaswa kujifunza kuwa na nia Thambiti.

Kushirikiana na Wengine.
Wahenga walisema kidole kimoja hakivunji chawa. Acha ubinafsi wa kufanya kazi pekee yako bali unapaswa kushirikiana na wengine, kushirikiana na wengine kunaweza kusaidia kufanikisha malengo yako hii kwa sababu unaposhirikiana na wengine mnabadilishana uzoefu pia.

Mengine tafuta kitabu usome ndugu
Siyo kila kitu lazima nikwambie bali mengine nenda katafute kitabu ili usome

Kufuata miongozo hii kunaweza kusaidia katika kufanikisha malengo yako na kufanya kazi kwa ufanisi.

Imeandikwa na Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments