BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha The 7 habits of highly effective people.


Mafunzo 8 kutoka kitabu "The 7 Habits of Highly Effective People" na Stephen R. Covey ni:

Kitabu cha 7 habits of higly efeective people kilichoandikwa na Spephen R. Covey kinaangazia mambo yafuatayo;

1. Kwenye kila jambo  unalolifanya basi hakikisha unakuwa mstari wa mbele, hii ikiwa na maana unapaswa kuchukua hatua za uwajibikaji kwa matendo. Usiwe mtu wa kusema nataka hili au nataka lile basipo kuchukua hatua kwani kufanya hivyo itakuwa ni kupoteza muda tu.

2. Unapopanga malengo yako, basi kumbuka kuweka malengo ya muda mrefu pia. Si kila kitu kitakupa matokeo ya haraka bali mambo mengine huchukua muda mrefu ili kuona matokeo yake. Hivyo mambo mengine yanahitaji uvumilivu wako ili uone matokeo.

4.  Jifunze kuwa na vipaumbele. Si kila jambo unatakiwa kulifanya, kwani kufanya hivyo utakuwa unafanya vitu kisha unaishia njiani, hakikisha unakuwa na vipaumbele. Yaani oredhesha vitu vya kufanya kwamba ukitoka jambo hili unakuja jambo hili. Epuka kuanzisha jambo kabla ya kutimiza jambo jingine.

5. Mwandishi anatuasa kwenye utafutaji wa majibu ya changamoto. Kwenye kila jambo unalolifanya pale unapokutana na changamoto yeyote ile basi hakikisha unakuwa ni mtu wa kutafuta  majibu ya kutatua changamoto husika.  Kuwa mtu wa kutafuta sababu kabla madhara hayajawa makubwa.

6. Kuwa mtu ambaye ni mzuri wa kusikiliza watu wengine pia. Unaposikiliza watu wengine ipo mitazamo mipya ambayo utaipata. Mitazamo hii mipya itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuweza kujenga fikra na mitazamo sahihi itakayokusaidia kwenye kila jambo ulifanyalo. 

7. Hakuna mafanikio utakayotengeneza peke yako. Mafanikio hutengenezwa kwa kushirikiana na watu wengine. Usiwe mbinafsi bali kubali kushirikiana na watu wengine kwenye kufanya kazi. Kumbuka ili upate matokeo makubwa kubali kushirikiana na wengine, ubinafsi hautakusaidia.

8. Kumbuka mafaniko huenda kwa mtu ambaye ameamua kuboresha afya yake ya kimwili, kiakili, kihisia, na kiroho. Ukiboresha maeneo hayo itakuwa ni rahisi zaidi kwako kupata kile unachokihitaji. Narudia tena ili uweze kuwa na ufanisi katika maeneo yote ya maisha yako kumbuka sana koboresha maeneo hayo niliyoyataja.

Natumai kuja jambo umejifunza. Asante kwa kusoma makala haya. Tukane kwenye uchambuzi mwingine.

Na; Benson Chonya!

Post a Comment

0 Comments