Kitabu cha Attitude is your superpower kilichoandikwa na Eduardo Clemente ni kitabu ambacho kinazungumzia mambo mengi yahusuyo mtazamo, mtazamo ambao unaweza kuyabadili maisha yako kwa kiwango kikubwa.
Yafuatayo ndiyo mambo utakayojifunza katika kitabu hicho!
Tabia inachora mtazamo.
Mwandishi Eduardo anaonesha ni kwa namna gani tabia yako inavyoathiri jinsi unavyojiona na unavyonekana na ulimwengu, inakuathiri katika uzoefu na fursa zako. Tabia yako inawaonesha watu wengine pia kuwa wewe ni mtu wa namna gani. Kwa mfano mtu akinyoa kiduku, ukimuona tu hivi kwa mara ya kwanza mtazamo wako tu juu ya mtu hiyo utakwambia huyo ni mtu wa namna gani.
Tabia yako huoneshwa na vile unayoonekana. Jenga tabia ambayo itachora mtazamo mzuri kwako na kwa watu wengine wanaokuzunguka pia.
Ujasiri huleta mafanikio.
Ujasiri wa mtu ndiyo nguzo uletayo mafaniko ya kweli, Ujasiri ukiongozwa na tabia chanya, unakupa nguvu ya kutenda na kufikia malengo yako. Nguvu ya ujasiri itakupa mafanikio ya kweli, acha kuwa muoga bali pambana ili kuyafikia mafanikio yale unayoyatamani kila wakati, kuwa jasiri ili uweze kufanikiwa zaidi.
Uchanya huwezesha uwezo
Kila mtu anatakiwa kuwa mtazamo chanya, mtazamo chanya ni chachu ya kupata kile ukitakacho, unapaswa kuwa na mtazamo chanya ili uweze kuchochea matumaini, uthabiti, na uwezo wa kushinda changamoto ambazo zinakusonga au ambazo zitajitokeza mbele yako.
Kukabili mawazo hasi
Mawazo hasi ndiyo yanayokwamisha au kupunguza kuendelea kupambana, inapotokea kuwepo hali ya mawazo hasi badilisha mazungumzo yasiyosaidia, anza mara moja kuzungumzia yale mawazo yaliyo chanya na imani za kuwezesha kuweza kulitimiliza jambo fulani na si kuendeleza kuzungumzia mawazo hasi yatakayokuendeleza mawazo hasi, mawazo yatakayokupa woga, mawazo yatakayokuondolea nguvu ya kuthubutu.
Kukubali mtazamo wa kukua
Inapotokea umepata mawazo yatakayokusaidia kukua zaidi unapaswa kuyachukua kwa mikono miwili mitazamo hiyo, kwa sababu mitazomo hiyo ni mali. Pia kila wakati amini katika uwezo wako wa kujifunza na kukua, inapotokea changamoto yeyote kwa kuwa wewe una mtazamo wa kukua basi chukua chongamoto hizo kama fursa ya kuboresha na kupata matokeo chanya zaidi.
Kuwa mtu wa shukrani
Mafaniko huenda mbio kwa mtu mwenye shukrani, unapaswa kuthamini vitu vizuri katika maisha yako, hata baraka ndogo unazozipata maishani mwako endelea kushukuru na si kukufuru. Ili kukuza mtazamo chanya zaidi ya yale yanayoendelea juu ya uso huu wa dunia hii basi wewe jifunze kuwa mtu wa shukrani, unapokuwa mtu wa shukrani ni kwamba milango mingi ya mafanikio hufunguka zaidi na zaidi pia.
Thibiti msongo wa mawazo.
Hili limekaa kisaikolojia zaidi, ambapo inashuriwa kuwa inapotekea una mawazo mengi zaidi basi jifunze mbinu nzuri za kukabiliana na hisia hasi na kuendelea na tabia chanya. Tabia chanya ndiyo itakayokusaidia kutoweka na tatizo hilo la msongo wa mawazo linalokukabili.
Weka malengo wazi na uweke picha ya mafanikio uyatakayo.
Ili uweze kujenga mtazamo chanya kuhusu mafanikio yako basi eleza matamanio yako na tumia tabia chanya kukuza safari yako. Chukua notebook andika malengo yako kisha andika pia mbinu za kutimiza malengo hayo. Kufanya hivyo itakusaidia kujenga mtazamo kama kile unachokitaka kinawezekana ama laah.
Kumbuka, tabia ni uamuzi.
Fanya juhudi kila siku kuchagua mtazamo chanya na wenye nguvu. Mtazamo chanya ndiyo utakao kupeleka nchi ya asali na maziwa endelea kuchakata ili uwe na mtazamo huo.
Kumbuka: Clemente anasisitiza kwamba kukuza tabia chanya ni mchakato endelevu. Kutumia mafundisho haya kwa ufanisi kunaweza kukusaidia kufungua uwezo wako, kufikia mafanikio makubwa, na kuunda maisha yenye furaha zaidi.
Asante tukutane kwenye maandiko ya kitabu kingine.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
0 Comments