BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Usichokijua kuhusu mambo unayojiambia kila siku.

Mambo unayojiambia mara kwa mara, mambo hayo yanageuka na kuwa uhalisia. Unatakiwa sana kuchunga mambo unayojiambia mara kwa mara. Kama kila wakati unajiambia huwezi au unaweza mambo hayo yataumbika ndani yako. 

Kila wakati unatakiwa kufikiria au kujiuliza, unajimbia nini hasa mara kwa mara. Mambo hayo unayojiambia mara kwa mara ndio hayo mambo yanakuja kutokea kwa nje na kuumba maisha yako. Kuwa makini na mambo unayojiambia.

Haiwezekani kila siku ujiambie, siwezi hili, siwezi lile, halafu ikatokea ukaweza, hicho kitu hakipo. Hakikisha, unajiambia mambo mazuri ndani yako, ya naweza, naweza, na utaweza. Ukijiambia mambo mazuri au mabaya yatatokea.

Uamuzi ni wako kipi unachotaka kujiambia mara kwa mara, ila kwa chochote utakachojiambia sana, kitakuwa kweli.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments