BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Njia za kupunguza ugumu wa maisha.

Ndugu, asikwambie mtu kufikia maisha ya mafanikio siyo kitu kirahisi kama wengi wadhaniavyo. Hii ni kwa sababu kufikia mafanikio ni lazima utakutana na panda na kushuka ndani yake. Hivyo kivyovyote vile unapaswa kuwa mvumilivu huku ukijituma kwa juhudi zote.

Ni muhimu kujituma kwa juhudi zote kwa sababu, kusema ukweli changamoto hazikwepeki unapotafuta mafanikio. Hivyo kila changamoto inapojitokeza kwenye kila jambo unalolifanya ni vyema ukajifunza namna sahihi ya kupambana na changamoto.

Kama nilivyosema hapo awali kwamba mafanikio hayajawahi kuwa rahisi hata siku moja. Hivyo unachopaswa kuelewa ni namna sahihi kupambana na ugumu huo. Hata hivyo watalamu wanasema maisha hayajawahi kuwa magumu ili sisi ndiyo wagumu, tunachotakiwa kufanya ni namna ya kuachana na ugumu huo tuliona na kuelekea mafanikio.

Pia njia nyepesi na rahisi ya kuachana na ugumu huo ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuachana na uvivu, kujitoa kikamilifu katika kufanya kazi mbalimbali sambamba na hilo tunatakiwa tuwekeze muda mwingi katika kujifunza mambo yatakayotusaidia kuweza kufanikiwa zaidi.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments