BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo utakayojifunza kutoka kwenye kitabu cha Your Next Five Moves.


Leo naomba tuangalie japo kwa uachacheyale yanayopatikana  katika kwenye kitabu "Your Next Five Moves" kilichoandikwa na Patrick Bet David lengo ni kujifunza ili tuweze kuboresha maisha yetu.


Kwenye kitabu cha Your Next five moves mwandishi anatukumbusha mambo haya:

Kuwa na mikakati ya mbele.
ili tuweze kupiga hatua kwenye maisha na mambo mbalimbali tuyofanyayo mwandishi anatatuasa tuweze kukiria hatua zako za baadaye na jinsi ya kufikia malengo yako.

Mwandishi hataki tupweteke na pale tulipo bali anataka tuweze kuwa na mikakati ambayo itatusaidia kuweza kufika mbele zaidi ya pale tulipo. Kwa nukta hiyo mwandishi anatutaka tuwe na malengo makubwa ambayo yanaweza kuyabidili maisha yetu kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Kutambua fursa.
Unapokaa mahali acha kufumba macho, bali macho yaweze kuona na kutambua fursa zitakazokusaidia kufanya jambo fulani lenye tija. Weka macho yako wazi kwa fursa mpya na za kipekee. Ukiona fursa fulani usione aibu kuifanya fursa hiyo, kitu cha msingi ni kuhakikisha fursa hiyo itakusaidia mkono wako kwenda kinywani.

Kujifunza kutokana na makosa
Kinachobadilisha maisha ya wengi ni kule kunakotokana na kuchukua hatua, huwezi kusema unataka kufanikiwa kama si mtu wa kuchukua hatua, ni lazima uwe mtu kuchukua hatua lakini pia kubali kujifunza kutoka kwa makosa yako na ya wengine ili uweze kutimiza yale yaliyo ya msingi katika maisha yako.

Kujenga mtandao
Kuwa na mtandao na watu sahihi katika maisha yako ni jambo la muhimu sana, ukitaka kufanikiwa zaidi hakikisha unajenge na unaendeleze mahusiano yenye manufaa na watu wanaoweza kukusaidia kufikia malengo yako.

Kuweka malengo yanayotimizika
Watakamu wa mambo wanasema unapopanga malengo basi hakikisha yakuwa ni malengo yanayotimizika, usipange malengo ambayo huwezi kuyatimiza. Weka malengo ambayo ni ya kweli na yanayoweza kufikiwa, kisha tengeneza mikakati ya kuyafikia au kuyatekeleza malengo hayo.

Kujiamini
Ngao ya mafanikio ya kila mtu hutokana na vile mtu hiyo anavyojiamini. Unapotaka kufanikiwa zaidi na zaidi unaoaswa kuwa na imani na uwezo wako na uwe tayari kushinda changamoto zozote zinazokuja. Hivyo unapaswa kujiamini zaidi na zaidi ili uwe kuweza kutenda mambo kwa ujasiri.

Kuwajibika.
Usipowajibika wewe mwenyewe juu ya maisha yako, amini hakuna mtu ambaye atakuja kuwajibika juu ya maisha yako. Unapojenga hali ya uwajibikaji basi  jisimamie mwenyewe na utendaji wako kutekeleza  malengo yako, malengo ambayo yatabadilisha maisha yako.

Kuendelea kujifunza
Maisha yanataka tujifunze kila ziku ili tuwe bora kila uchao, hivyo ili maisha yako yawe bora basi kuwa tayari kujifunza kutoka kwa uzoefu wako na kuendelea kukuza ujuzi wako kila siku. Unapojifunza kila siku unakuwa mbobezi wa mambo, endelea kujifunza.

Kuwa na uvumilivu.
Safari ya kufikia malengo yako inaweza kuwa ndefu na yenye changamoto, hivyo kuwa na uvumilivu na subira ni muhimu. Unapokuwa mvumilivu unajifunza mengi pia.

Jambo jingine nenda kasome kitabu🤣
Usipende maisha ya kuteleza, nenda kasome mwenyewe kitabu hicho.

Kitabu Your Next Five moves ni kitabu kizuri cha kujifunza na kusaidia katika safari yako ya maendeleo binafsi na kitaaluma, kitafute kitabu hiki ili uweze kujifunza mengi zaidi.


Na; Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments