BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kijue Kitu Hiki, Utafanikiwa.

 


Hata siku moja, usijaribu kukijua kitu chochote kwa akili yako na hisia zako. Kijue kitu kwa kutenda, kijue kitu kwa kukiishi, kijue kitu kwa kukifanyia kazi.

Watu wengi wanashindwa kwenye maisha sababu wanajua mambo nusunusu au juu juu tu. Ukitaka kufanikiwa, chochote kile unachokifanya, kijue kwa uzoefu wako wote.

Usikubali kufanya mambo yako kwa akili au hisia tu.  Ingia kwa undani katika uzoefu wa kila wakati, uzoefu wa hatua kwa hatua, ili kujua moja kwa moja kwa undani kile ukifanyacho na utaona muujiza wa mafanikio yako.

Kama nilivyosema kila wakati kijue kitu chochote zaidi ya mawazo, hisia au mihemko uliyonayo. Kijue kitu hicho kwa kutenda, kukiishi, na pia kijue kwa kukifanyia kazi. Ukiweza kufanya hivyo, utafanikiwa.

Imeandikwa Na Melisa Kawa wa Dar Es Salaam, Tanzania.

Mawasiliano 0745268398


Post a Comment

0 Comments