Ni ngumu sana na haiwezekani nguvu zako unazozitoa, eidha ziwe ninaenda kwenye malengo yako au zinaenda popote, zikaenda bure.
Ni lazima nguvu zako zirudi kwa namna yoyote ambayo hata wewe huijui.Kwa mfano, unapotumia tochi usiku, lazima ikutane na giza.
Pia unapotoa nguvu zako kuwasaidia watu au kuwaumiza watu kwa namna yoyote ile, lazima nguvu hizo zitakurudia wewe tena wakati mwingine bila kujua.
Hivyo unatakiwa ujue, kila kitu kina uwezo wa kurudi kwetu tena. Kama jibu ni hivyo unatakiwa kuzitumia nguvu zako kwa umakini, isije ukazitumia kwa hovyo zikakupoteza na wewe na ukashangaa hufanikiwi.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu

0 Comments