BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Chagua maisha ya namna hii ili ufanikiwe.



Maisha tunayoishi ni matokeo ya uchaguzi wetu. Kile unachochagua au kwa jinsi unavyochagua uishi ndio maisha utakayokuwa nayo.

Kwa kuwa iko hivyo, nikushauri tu, kila wakati chagua kuishi maisha ya hali ya juu. Acha kujichagulia kuishi maisha ya chini ya wasio jiweza. Amua kuishi maisha ya 'level' za juu.

Una haki ya kuishi maisha hayo, kwa sababu ndani yako una nguvu, na una uwezo wa kutengeneza maisha uyatakayo. Pia kwa kila muda ukiishi kwa ubora na kutumia fursa vizuri, basi utaweza kuishi maisha ya hali ya juu.

Kipi kinachokukwamisha, amua leo kuanza kutengeneza na kuishi maisha bora ya hali ya juu. Maisha hayo mazuri yapo kwa ajili ya wewe na sio watu wengine tu peke yao.

Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments