Kitabu hiki cha Herbet Harris kinazungumizia sheria ambazo zinafanya kazi ulimwenguni kote ambapo kama utaamua kuzifanyia kazi zitakusaidia kuwa bora zaidi na hatimaye kupata kile unachokihitaji, kwa maana ya kufanikiwa.
Kwenye kitabu hicho haya ndiyo yaliyosisitizwa zaidi;
1. Sheria ya Imani.
Sheria ya kwanza ni jifunze kuwa mtu mwenye imani. Jenga imani imara ndani yako na uwezo wako wa kufikia malengo yako. Usipokuwa na imani thabiti juu ya mambo chanya kuhusu mafanikio ni kwamba mafanikio yatajitenga nawe. Pia mwandishi anatuasa sana kuepuka kuwa na mawazo hasi kwani mawazo ndiyo ambayo huzuia mafanikio ya wengi.
2. Kuweka Malengo.
Kanuni nyingine itakayokupa mafanikio ni wewe kuamua kuweka malengo. Kwenye hili mwandishi anatuasa sana tuweke malengo wazi kwani endapo utakuwa mtu ambaye unaweka malengo wazi itakuwa ni rahisi sana kufanikiwa. Pia mwandisi anasema kwenye kuweka malengo wazi ni lazima uwe na lengo maalumu, yaani lengokuu huku lengo hilo ukiliandika sehemu, kwani unapoandika inakupa mwelekeo wa kile unachokitaka.
3. Sheria ya Matarajio Chanya
Kwenye kila jambo lako lolote lile jifunze kuwa na matarajio chanya. Unapokuwa na matarajio chanya inakupa nguvu na hamasa ya kuweza kupambana zaidi. Maisha yanakutaka uendelea kuwa na mtazamo chanya ili uweze kuyavuta mafanikio na fursa pia wakati mwingine kuwa na matarajio chanya yanakusaidia sana namna bora itakayokusaidia kupambana na changamoto zako.
4. Sheria ya Kuchukua Hatua.
Maisha ya mafanikio yanapinga sana kuwa ni mtu wa matamanio tu pasipo kuwa mtu wa kuchukua hatua, usiishie kutamani bali kuwa mtu wa vitendo zaidi juu ya yale unayoyatamani. Usiwe tu na ndoto chukua hatua thabiti kuelekea malengo yako, hata kama ni ndogo. Maendeleo yanajengwa kwa hatua, siyo tu kupanga au kusema sema tu. Chukua hatua ili uweze kufanikiwa.
5. Sheria ya Kujituma.
Sheria ya kujituma inasema kujituma kunalipa zaidi. Kwenye kila jambo wewe jitoe kikamilifu, fanya kazi kwa kujituma kikamilifu. Pamoja na uwepo wa vikwazo na changamoto ambazo utakuna nazo unapaswa kujituma ili uweze kuwa hodari. Kujitutuma ndiko kutkakokusaidia sana kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine. Jitume bila kuchoka ili uweze kupata kile unachokihitaji.
6. Sheria ya Mienendo.
Mienendo ni tabia. Hivyo mwandishi anasema kila wakati ili tuweze kufanikiwa zaidi tunapaswa kujenga mienendo mizuri ambayo itatupa mafanikio tuyatakayo. Jenga mienendo chanya inayolingana na malengo yako na mtazamo wa mafanikio. Kurudiarudi kufanya jambo husaidia kutengeneza tabia chanya, hivyo kuwa na tabia ya kurudiarudia kufanya jambo kutakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuweza kupata matokeo tarajiwa.
7. Sheria ya Akili ya Kinafsi.
Sheria hii inakutaka sana kuwa mtu ambaye unajijengea kauli nzuri ambazo zikusaidia kupambana zaidi. Kila uwapo pekee yako jenga taswira chanya juu ya kile unachokitaka, pia kila wakati jifunze kujenga mazungumzo chanya ndani ya nafsi yako huku ukiamini kuwa kila jambo linawezekana. Yale unayoyawaza zaidi ukiwa peke yako hugeuka kuwa kitu halisi.
8. Sheria ya Kutoa na Kupokea.
Sheria hii inatutaka zaidi ujikite katika kusaidia wengine na kutoa thamani. Mafanikio mara nyingi hutokana na kutumikia wale walio karibu nawe. Sheria hii inafanya kazi sana kwamba kama wewe utakuwa ni mtu wa kupokea pekee pasipo kutoa ni kwamba kufanikiwa kwako itakuwa ngumu sana hivyo jifunze kutoa zaidi kwa wahitaji ili nawe uweze kupata zaidi.
9. Sheria ya Shukrani.
Shukuru kwa kila jambo, mtu akikupa kitu shukuru. Ipo nguvu kubwa sana katika shukrani ambapo kanuni hii inasema unapokuwa mtu wa shukrani unabarikiwa zaidi. Hivyo kila wakati unaaswa sana kutokaa kimya bali unapaswa kujenga mtazamo wa shukrani. Jenga mtazamo wa shukrani kwa ulicho nacho tayari ili kuvuta zaidi mafanikio katika maisha yako.
10. Sheria ya mahusiano mazuri na wengine.
Jenga mahusiano mazuri na watu wengine. Kwenye hili mwandishi anatukumbusha mambo mawili kwanza, ni kushirikiana watu wengine katika kufanya kazi, jambo la pili mwandishi anatukumbusha kuweza kuwa na mahusiano imara na watu wengine, mawasiliano hayo ni azima yawe chanya yenye msukumo mkubwa katika suala la kuleta maendeleo ya kila mmoja wetu.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya!
Tukutane kwenye uchambuzi wa kitabu kingine, jumapili ijayo muda wa Tisa kamili jioni, hapa hapa Mafanikio App!
0 Comments