BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kila fedha unayoipata hakikisha inagawika kwenye makundi haya matatu.



Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa na the school of Academia kuhusu masuala ya fedha waliwahi kusema kuwa, ili mtu awe na mafanikio ya kifedha basi mtu huyu anatakuwa ajifanyie tathimini na uchambuzi yakinifu kuhusu hali yake ya kifedha.

Hii ikiwa na maana kila upatapo fedha ni lazima uwaze namna utakavyoitumia fedha yako. Usitumie fedha yako bila utaratibu kwani kufanya hivyo mwishowe utakuja kugundua hakuna jambo la maana unalolifanya, kwani kila fedha utakayokuwa unaipata itakuwa inapotea bila habari.

Kumbuka pia kila fedha unayoipata inaweza kugawika kwenye makundi matatu, yaani matumizi, akiba na uwekezaji. Ukiona pesa yeyote unayoipata haiwezi kugawika kwenye makundi hayo matatu basi fahamu kuwa ni lazima utakuwa na changamoto ya kifedha.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments