Mwanadamu awe yote mara nyingi husongwa na kitu kinachoitwa hofu kwenye maisha yake. Hofu ni adui mbaya hasa pale linapokuja suala la uthubutu wa kufanya mambo yenye tija katika maisha.
Wengi wao hudhani wapo sahihi kutokuchua maamuzi sahihi, kumbe ukiwaangalia watu hao wanashindwa kuchukua maamuzi sahihi kwa sababu ndani yao wamesongwa na hofu.
Hofu ambazo zimewasababisha watu hao kuwa ni waoga wa kuamua kuchukua maamuzi ya kufanya yale yaliyo na tija.
Leo hii watu wanaogopa kuweka akiba za fedha huku wakihofia kuibiwa au wengine ukiwaambia waweke akiba, watakujibu niweke akiba nikifa je? Pesa zangu atatumia nani? Kwa mfano huo utaona ni kwa namna gani watu walivyojengwa na hofu ndani mwao hata wakafanya yale yaliyo ya muhimu.
Sasa katika maisha haya ili uweze kufanikiwa zaidi na zaidi basi unatakiwa kuishinda hofu iliyojenga ndani mwako, hamasa ya kushinda inatakiwa kuwa kubwa kuliko hofu ya kushindwa.
Ishinde hofu ili uweze kufanikiwa.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya

0 Comments