Fursa zipo kila mahali, ila changamoto huwa inakuwa kwetu ambao tumezungukwa na fursa hizo. Wengi wetu hudhani fursa ni kitu ambacho kipo wazi wazi kama wengine wadhaniavyo, hapana fursa hazipo hivo.
Fursa huwa zina tabia za kujificha, ambapo ili uweze kuziona fursa hizo unatakiwa kufanya uchunguzi yakinifu juu ya fursa hizo. Vile vile fursa mara nyingi huwa zina tabia ya kuona aibu ambapo zinasubiri uzifuate zilipo.
Robert kiyosaki aliwahi kusema "umaskini ni kupitia kwenye fursa kila wakati".
Ikiwa una changamoto ya kutokuona fursa kwenye eneo fulani basi hakikisha anatafuta majibu ya changamoto fulani katika eneo husika, hapo utakuwa umewaza kuiona fursa husika ambayo mwanzo ulikuwa huioni.
Na; Benson Chonya.

0 Comments