BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Changamoto pekee inayoyakumba maisha ya wengi.

Miongoni mwa changamoto kubwa zinayoyakumba maisha ya wengi ni kwamba wengi wetu tunakosa ujasiri wa kuthubutu na kufanya mambo mbalimbali yaletayo maendeleo katika maisha yetu.

Changamoto hii imekuwa ni kubwa sana kwa kizazi hiki. Wengi hupata mawazo mazuri ila wengi huishia kwenye hatua ya awali yaani ya kuwaza tu, wengi hawawezi kubadili kile wakiwazacho kwenda katika matendo kwa sababu ya kukosa ujasiri wa kujiamini.

Wengi hutawaliwa na mawazo hasi, wengi hudhani haiwezekani, ila ukweli ambao upo bayana ni kwamba ukiweza kujijengenea uwezo wa kujiamini kwenye kila jambo, basi mafanikio makubwa yatakuwa upande wako.

Na ili uweze kujijengea uwezo huo wa kujiamini unatakiwa kuwa na vitu viwili muhimu ambavyo ni, maarifa sahihi ya kile unachokifanya au unachotaka kufanya au unapaswa kuwa na uzoefu katika jambo husika. Ukiweza kuyafanikisha mambo hayo utaondokana na tatizo la kutokujiamini.

Na; Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments