BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Athari utakazozipata ukiwa ni mtu kughairisha mambo ya msingi.

 


Kwa kingereza kitendo cha kuairisha kufanya mambo ya msingi  huitwa Procrastination, Procrastination  ni ile hali ambayo anakuwa nayo mtu ya kuahirisha kufanya baadhi ya mambo muhimu kwa wakati sahihi. Hali hii huwakumba watu wengi sana, tunaweza kusema huu ni ugonjwa ambao umewapata watu wengi.

Ugonjwa huo wa kuarisha mambo unazidi kukua kwa kasi sana siku hadi siku kwa  sababu wengi  huwa tunaamini kuwa tuna muda wa kutosha wa kufanya mambo hayo tuliyoyagharisha kwa hapo baadae kumbe siyo kweli muda huo unakuwa siyo rafiki.

Ukiwa na tabia hii ya kughairisha kufanya mambo ya msingi unakuwa kama umeingia kwenye uraibu wa hali fulani, yaani unakuwa kila ukipanga kufanya jambo fulani hata iweje unajikuta unaghairisha kwa sababu tayari unakuwa una uraibu wa kughairisha kufanya mambo fulani ambao upo tayari ndani yako.

Sasa ikiwa utaendeleza tabia hii ya kughairisha mambo utapata athari zifuatazo;

1. Utapitwa na fursa lukuki.

Unapokuwa na tabia ya kughairisha kufanya mambo ya msingi unakuwa unapitwa na fursa lukuki ambazo kwa wakati wa kughairisha hukuweza kulitambua hilo. Wale walio mahodari wa  kuairisha mambo hupitwa na mengi mazuri.

Kwa mfano kama umepanga kulima kilimo cha aina fulani wewe lima, kwa sababu kuna watu huwa wanakuja kujilaumu mbeleni kwamba dah wakulima wenzangu wanapata faida sana hivi sasa, kwa nini niligharisha kulima?

Wakati unayasema hayo kumbuka tayari unakuwa umekwisha chelewa na fursa hiyo inakuwa tayari imeshakupita juu ya kichwa chako. 

Hivyo kwenye kila eneo ambalo unaliona ni la muhimu kwako kulifanya ni heri ulifanye hivi sasa ili kuepuka majuto ya hapo baadae kwamba  " ningejua...ningefanya kipindi kile".

2. Unapoteza muda mwingi kwenye vitu visivyo vya maana.

Waairishaji wengi kupoteza muda wao mwingi kwenye vitu visivyo maana. Wao imani yao kubwa huamini kuwa wanao muda wa kutosha wa kufanya mambo fulani.

Kumbe kuamini huko, ni kama vile kuonja asali, kwani tatizo lao la kugharisha mambo huzidi kukua na kukomaa kadri siku zinavyozidi kwenda. Hivyo kila wakati wakitaka kutekeleza jambo fulani hujiambia nitafanya siku nyingine na hata hiyo siku nyingine jambo hilo pia halitafanyika pia.

Mwishowe, wanajikuta watu hao wanapoteza muda mwingi sana kwenye vitu ambavyo  walipaswa kuvifanya mapema zaidi.

Au wakati mwingine huwa wanatumia muda mwingi kwenye vitu visivyo na tija huku vile vyenye tija wakiamini watakuja kuvifanya hapo baadae, na hapo ndipo tatizo la kughairisha mambo ambapo huanzia.

Zipo athari nyingi za kughairisha mambo hizo ni baadhi tu ya atahari hizo, hivyo ili kuepuka kupatwa na athari hizo usiwe ni mtu wa kugaharisha mambo kwani kuendelea na tabia hiyo ni kwamba utapitwa na vitu vingi sana vyenye kukuleta majuto makubwa maishani.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.
0747030303

Post a Comment

0 Comments