Mahitaji
1.
Siagi 1 cup
2.
Sukari 1 cup
3.
Mayai 2
4.
Unga wa ngano vikombe 4
5.
Baking powder 1 tsp
6. Arki(essence) unayopenda 1 tbsp ..nimetumia arki ya banana
Saga sukari na siagi mpaka ichanganyike vizuri,
tia yai 1 zima , la pili tia kiini tu , ute weka pembeni ,endelea kusaga kwa
dakika 1 mpaka 2 ,weka baking powder na arki/essence, saga tena kidogo anza
kutia unga wa ngano kidogo kidogo mpaka unga unashikana linakua donge gumu la
kiasi ,nimetumia unga vikombe 4, Ila muhimu angalia donge lishikane kiasi .
Weka sehemu kama kibao cha kukatia maandazi ,usukume unga kama chapati Ila
usiwe mwembamba sana,tumia kitu chochote kukata(unaweza kufanya shape unayopenda)
nimetumia glass kukatia. Ukimaliza zote kuzikata ziweke kwenye trey upake ule
ute wa yai juu ,bake mpaka vinawiva,..
vitoe
Iyo ya juu ni chocolate, yayusha milk chocolate na maziwa au double cream then tia kwenye piping bag au kitu chochote ambacho itatoka nyembamba uchoree juu . Sio Lazima uweke chocolate juu.
Nimetumia arki ya banana ambayo ilileta rangi
hiyo ,ukitumia arki nyengine mfano vanilla inaweza kutokea rangi tofauti kidg
Ila haina tatizo.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya kwa msaada wa
mtandao.
0 Comments