Moja kati ya vitu muhimu sana kwenye maisha yako ambacho kitakutenga mbali na umaskini ni pamoja kuendelea kujipa hamasa wewe mwenyewe za kuweza kufanya zaidi na zaidi.
Usisubiri hata siku moja hamasa kutoka kwa mtu mwingine ndipo uchukue hatua ya kuanza kufanya kitu fulani hapo utakuwa unajichelewesha wewe mwenyewe, vipi kama mtu unayemsubilia akupe hamasa asipotokea si ndiyo kufa kwako kutakapoanzia.
Unapaswa kukumbuka kuwa hamasa ya kweli na yenye kuleta mafanikio huanza na mtu mwenyewe, hivyo anza kujipa hamasa mwenyewe za kiutendaji kwenye kila jambo ulifanyalo au unalotaka kulifanya.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments