BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo hili ni muhimu sana kwenye kila maisha ya mmoja wetu.

Ni bora kukosa chakula lakini siyo kukosa tumaini.Tumaini ni bora kuliko chakula. Ni muhimu kuwa na matumaini na  wakati ujao kuwa hali yako itakuwa bora licha ya hali yako ya sasa ya maisha ni ngumu.

Madhara ya kukosa tumaini ni makubwa kwani jinsi unavyopoteza tumaini ndivyo unavyopoteza siku zako za kuishi hapa duniani. Ukikosa matumaini na mafanikio yako unayakosa pia.

Ukikosa matumaini ndivyo unajikuta unavyojiingiza zaidi katika madawa ya kulevya , vilevi na mambo mengine yanayohusiana na hayo. Mpaka hapo unaona kukosa matumaini kulivyo kubaya na kunatisha.

Mtu aliyekosa tumaini la maisha ni kama tayari ameshakufa anasubiri tu kwenda kuzikwa.Hata kama uko katika hali ngumu kiasi gani ila usichoke kuwa na tumaini la maisha yako mwenyewe.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments