Mahitaji:-
1. Maziwa lita 5
2. Maji ya madafu au ya kawaida safi ya kunywa lita 1 1/2
3. Sukari kiasi chako
4. Hiliki ya unga kijiko 1 cha chakula
5. Vanilla vijiko 3 vya chakula
6. Cornstarch/cornflour 1/4 kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Tia maji,hiriki pamoja na cornstarch katika sufuria ,koroga vizuri kisha injika jikoni juu ya moto wa kiasi, pika ukiwa wakoroga hadi uone imefanya uzito. Epua
2. Tia mahitaji yalobaki kisha koroga vizuri vichanganyike.
3. Mimina katika vifuko vya ice cream kisha gandisha kwa masaa 6 au hadi zipate kuganda.
4.Kisha nenda kauze maeneo ya shule na sehemu zenye mikusanyiko ya watu kama stendi,sokoni,viwanja vya mipira kwa bei ya 100 au150
Note:- Cornstarch si lazima ila kwa wanaopenda ice cream laini weka ndio kilainishi chenyewe
Unaweza tumia radha upendazo pia unaweza weka rangi kuleta mvutu tofauti, kwa za maziwa rangi ya manjano ya mbali yapendeza au orange ya mbali.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya kwa msaada wa
mtandao.
0 Comments