BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUTENGENEZA MANGO ICE CANDY/ PIPI ZA BARAFU ZA EMBE (ICE CREAM

 


Mahitaji:-

1. Embe 6 kubwa zilizomenywa na kukatwa katwa

2. Sukari 1/4 kilo au kiasi chako

3. Maji lita 3 au zaidi

4. Cornflour vijiko 2 vya chakula

5. Maji ya ndimu 1/4 kikombe

NAMNA YA KUTAYARISHA

1.  Tia 1/4 lita ya maji katika sufuria pamoja na cornflour ,koroga vizuri kisha injika jikoni pika juu ya moto wa kiasi ukiwa wakoroga hadi ifanye uzito. Epua

2. Acha mchanganyiko upoe kidogo kisha mimina katika blender pamoja na embe, sukari na maji 1/2 lita saga hadi mchanganyiko uwe laini kabisa.

3. Mimina katika bakuli tia mahitaji yalobaki ,koroga vizuri kisha funga ice cream zako kama kawaida. 

4. Acha zigande katika freezer kwa muda wa masaa 4 au hadi zipate kuganda vizuri tayar kwa matumizi.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya kwa msaada wa mtandao.


Post a Comment

0 Comments