BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUTENGENEZA KARANGA ZA KASHATA



1.      Karanga   Kilo 5

2.      Sukari     vikombe 2

3.      Maji vikombe  1

4.      Maziwa ya unga  2 vijiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

1. Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.

2. Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.

3.  Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.

4. Paka mafuta treya  kisha mimina na utandaze upesi upesi.

5. Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.

Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya kwa msaada wa mtandao.


Post a Comment

0 Comments