Ipo sauti mbaya sana ambayo yenyewe kazi yake kubwa ni kuwanong'oneza watu kuwa hawawezi kufanikiwa kwenye mambo fulani ya maana.
Sauti hii ina ushawishi mkubwa sana, inawafanya watu wawe waoga sana ambapo kila wakati huwajaza watu hao hofu. Hofu ambayo huwafanya watu kile walichokiwaza wasikiweke katika matendo.
Kwa mfano unaweza ukawaza namna utakavyoanza kuweka akiba. Ukiwaza hivyo ndipo ile sauti yenye kuogofya na kuleta hofu inapokujia na kukufanya uone ni kwa namna gani ugumu wa jambo hilo ambavyo haliwezekani, mwisho wa siku unaachana na wazo lako la maana.
Sasa ili uweze kuishinda sauti hiyo yenye hofu ndani yake huna budi kuvaa ujasiri wa hali ya juu kila wakati sauti hiyo inapokujua, amini ya kuwa unaweza kufanikiwa haijalishi kuna changamoto za aina gani ambazo utakuna nazo.
Pia ili uishinde sauti hii ambayo hukutisha tamaa watu wengi, jifunze kugeuza yale uyawazo katika matendo kwa haraka zaidi.
Acha kuwaza mambo kisha ukayaacha.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya
0 Comments