Wengi hujivuta vuta mwisho wa siku fursa hizo huchukuliwa na watu wengine huku wao wakibaki wanashangaa tu.
Sasa ujumbe huu uwe mahususi kwako kwamba kama unataka mafanikio ya viwango vya hali ya juu maishani mwako hususani suala la kutengeneza fedha nyingi zaidi basi unapaswa kuwa tayari kuchua hatua za haraka kila unapoona fursa ya maana.
Haupaswi kujivutavuta kila unapoona fursa kwani ukifanya hivyo utazidi kubaki nyuma kama ulivyo mkia.
Pia ikumbukwe kuwa utamu wa maisha utauona endapo utaacha tabia ya kugharisha kufanya mambo yaliyo ya msingi maishani mwako. Yafanye yale yaletayo tija kwa vitendo.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya
0 Comments