Kama leo hii nikiulizwa bahati ni kitu gani? naweza nikasema kuwa bahati ni kitu adimu sana, au bahati katika maisha haipo kwa mtu aliyembweteka bali ni matokeo ya juhudi zako binafsi katika kufanya jambo fulani.
Mtu yeyote ambaye leo hii unamuona ana bahati, ukimuuliza mtu huyo hata sema kuwa ana habati bali atakwambia mchakato aliuotumia mpaka kumuona kuwa ni mtu mwenye bahati.
Kwa nukta hiyo, ndipo ninaporudia kuwa mchakato huo ndiyo juhudi binafsi zilizomsaidia kuweza kufanikisha jambo fulani. Hivyo hata wewe ili uweze kufanikiwa zaidi na zaidi acha kuamini kuwa kuna bahati kwenye maisha pasipo juhudi binafsi, bali ni matokeo yako ya kiutendaji ndiyo yatakayokupa mafanikio.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya
0 Comments