BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Zingatia hili ili uone faida kwenye biashara yako.

Biashara yoyote ile ili uone faida yake ni lazima uangalie uwiano wa faida katika biashara (profit margin). Uwiano katika biashara mara nyingi huangalia uwiano wa kuchukilia biadhaa na bei ya kuuzia biadhaa hiyo.

Kwa mfano zipo bidhaa zenye uwiano wa faida  (profit margin) ambazo ni kubwa. Kwa mfano unaweza kuchukua biadhaa kwa shilingi elfu nne(4,000) kisha wewe ukaja kuuza kwa shilingi elfu nane (8,000). 

Kwa mfano huo hapo uwiano wa faida (profiti margini) ni shilingi elfu nne (4,000) hiyo ni faida kubwa. 

Lakini zipo bidhaa ambazo uwiano wa faida ni mdogo (profit margin). Kwa mfano unaweza ukanunua bidhaa ya shilingi elfu nne (4,000) kisha ukaja kuiuza bidhaa hiyo kwa shilingi elfu nne na mia tano (4,500) profit margin ni shilingi mia tano (500) ambayo ni faida ndogo ukilinganisha na mfano wa kwanza.

Kwa mifano hiyo niliyokueleza bila shaka nadhani umeelewa ni nini ambacho namaanisha. Ukuaji wa mtaji wako mara nyingi ni lazima uzingatie jambo hilo la uwino wa faida katika bidhaa unazoziuza ili uweze kukua zaidi na zaidi.  

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments