BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kuzingatia ili uweze kupata faida kwenye biashara yako.

Ili uweze kupata faida kubwa kwenye biashara yako basi yakupasa kuangalia sana bidhaa zenye mzunguko mkubwa. Yaani angalia biadhaa zenye uhitaji mkubwa ambapo utokaji wake ni wa mara kwa mara.

Ukifanikiwa kuangalia jambo hili kwa umakini mkubwa, huenda ukaona mabadiliko makubwa sana kwenye biashara yako hususani suala la ongozeko la mauzo.

Na ili uweze kufanikiwa katika hili epuka sana kuagiza bidhaa kwa maono yako binafsi, bali agiza bidhaa kwa ajili ya kufanya biashara kutokana na mahitaji ya wateja wako.

Angalia biadhaa ambazo wateja wanaulizia mara kwa mara kisha anza kuuza. Acha kuuza bidhaa zenye mzuko mdogo kama mtaji wako ni mdogo kwani huenda usione faida itokanayo na biashara hiyo, bali kama mtaji wako ni mdogo uza bidhaa zenye mzunguko mkubwa.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments