BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo litakalokusababisha pesa zako zikukimbie.

Jambo pekee ambalo litakufanya pesa zako zikukimbie kila wakati ni kutaka kupata faida kubwa kwa haraka kuliko kiwango chako cha mtaji ulichowekeza. 

Jambo hili limewafanya watu wengi waishiwe na pesa zao bila wao kujua, wapo watu leo hii wanataka kuwekeza shilingi elfu moja ili wapate laki saba ndani ya masaa ishirini na nne.

Kitu hiki kimesababisha watu wengi wapoteze fedha zao nyingi bure. Sasa ikiwa unataka mafanikio ya kifedha unatakiwa kujua utaratibu wa uwekezaji wenye mafanikio haupo hivyo.

Bali unatakiwa kuwa mvumilivu, acha tamaa za namna hiyo kwani kutanguliza tamaa za kutaka utajiri wa namna hiyo ni kupoteza fedha zako bure. Kuwa makini katika hili. 

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya. 

Post a Comment

0 Comments