Kila wakati unao uchaguzi, eidha
uchague kufanya mambo mepesi ambayo hayaleti mabadiliko ya maisha yako au
uchague kufanya mambo magumu yatakayoleta, mabadiliko ya maisha yako.
Kwa mfano, kulalamika ni kwepesi lakini kwako hakuna msaada, badala yake ni bora ungechukua hatua. Kuchelewa kuamka ni rahisi, lakini hakuna unachopata bora ungewahi kuamka maana ungefanya kazi zako kwa ufasihi na ubora.
Wale wote wanaoendelea kuchagua mambo rahisi, basi wanaoendelea kuwa watumwa wa maisha yao. Kuendelea kufanya mambo rahisi ni hatari na utumwa mkubwa kwako. Pia mambo hayo rahisi hayawezi kukufanikisha.
Kama
unataka kujenga maisha yako ya kesho na yakawa ya mafanikio. Anza sasa, kufanya
mambo magumu na achana na kufanya mambo mepesi yasiyo na msaada kwako.
Mambo mepesi yatakupoteza usipokuwa makini.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments