Mafanikio hayaendi kwa watu wanaosubiri hali au mazingira yawe kamili. Mafanikio yanaenda kwa watu wanaoamua kufanya kwa yale waliyonayo, na kwa wakati wa sasa na sio kusubiri wakati wowote ule.
Mafanikio hayaendi kwa watu wanaosema wako 'bize' na hawana muda, na watafanya kesho au muda mwingine. Mafanikio yanaenda kwa watu wanaojitoa kutafuta muda na kuchukua hatua za kufanya.
Kama wewe ni bado wa kusema huna muda, utafanya kesho, basi nikwambie mafanikio tayari yamekupiga kikumbo cha kwaheri. Mafanikio hayataki watu wa namna hiyo kabisa, yanataka uchukue hatua.
Unatakiwa ujue mafanikio hayasubiri mtu na hayasubiri hali yoyote iwe nzuri. Ni jukumu lako wewe kutengeneza mazingira yatakayokusaidia katika kufanikiwa kwako na sio mtu mwingine bali ni wewe.
JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYIA KAZI, elewa mafanikio hayaendi kwa
wanaosubiri kesho au kusubiri mazingira yawe bora. Mafanikio yapo kwa
wanaochukua hatua sasa, chukua hatua, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia
WhatsApp.
0 Comments