BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo utakayojifunza kwenye kitabu cha Richest Man in Babylon.


Kitabu cha "Richest Man in Babylon" au kwa kiswahili tajiri wa babeli ni miongoni mwa vitabu vyangu pendwa vya siku zote. Kitabu  kimejaa wingi wa  mafundisho muhimu kuhusu uwekezaji, usimamizi wa pesa, na mbinu maridhawa zitakazokusaidia kupata fedha.


Naomba nikuletee japo kwa uchache mambo muhimu utakayojifunza ambayo yameandikwa katika kitabu hichi kama ifuatavyo ;

Kutenga sehemu ya mapato yako kwa ajili ya uwekezaji. 
Mwandishi anatusisitiza sana kuweka kando sehemu ya mapato yetu kwa ajili ya uwekezaji ili kuweza kujenga utajiri na uhakikishe ustawi wa baadaye.

Kujifunza na kuendeleza ustadi wa kifedha. Mwandishi unatuelimisha kwa kina kuhusu njia bora za kusimamia pesa zako na jinsi ya kufanya uwekezaji mzuri ambao utakupa faida.

Kuwa mwaminifu kwa wengine katika biashara. 
Kuwa mwaminifu na waadilifu katika shughuli zako za kifedha itakusaidia kupata imani na uaminifu wa wengine, ambayo ni muhimu katika biashara. Bila uaminifu kwenye maisha yako kila kitu kitakuwa ni kitu kigumu sana kwako.

Kuwekeza katika miradi yenye faida.
Chagua na wekeza katika miradi ambayo ina uwezo mkubwa wa kurudisha faida nzuri. Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu kama hautakuwa makini ni kwamba kila uwekezaji wako utakuwa unakupa matarajio ambayo ulikuwa huyatarajii au uwekezaji wako utakupa hasara.

Kujifunza kutokana na makosa
Jifunze kutokana na makosa yako, na si kukata tamaa za kiutendaji, tumia makosa yako kama fursa ya kujifunza na kuboresha mbinu zako za kifedha. Makosa ni shule ya kuinuka upya na kujenga mafanikio yaliyo sahihi kwa mtu anayelewa thamani ya makosa hayo.

Kudhibiti matumizi yako 
Hakuna shule inayofundisha namna sahihi ya kudhibiti matumizi yako ya kifedha isipokuwa wewe mwenyewe kuamua kudhibiti matumizi hayo,  kitabu hiki kinatutaka tupunguze matumizi yasiyo ya lazima pia tuwe na utaratibu wa kuweka akiba na kuwekeza zaidi kwa ajili ya ustawi  wa kifedha.

Kuweka malengo ya kifedha
Pamoja na kupanga malengo mengine jifunze pia kuweka malengo ya kifedha. Malengo ya kifedha ni muhimu kuwa nayo kwani husaidia pia kuyatekeleza malengo mengine. Weka malengo ya kifedha na jitahidi kuyafikia kwa nidhamu na bidii.

Kuwekeza katika elimu yako binafsi 
Tumia muda na rasilimali kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji na usimamizi wa pesa ili uweze kufanya maamuzi bora ya kifedha. Uwekezaji binafsi ni ule ambao utaendelea kukupa elimu ya fedha. Uwekezaji huo ni kama vile kununua vitabu vinavyofundisha elimu ya fedha.

Kuwa na uvumilivu
Hakuna mafanikio ya kulala maskini na kuamka tajiri, bali mafanikio ni mchakato hivyo jifunze kuwa mvumilivu sana huku ukiendelea kupambana. Unapaswa kuelewa kuwa Uwekezaji wa muda mrefu mara nyingi unahitaji uvumilivu na subira ili kuona matokeo mazuri.

Mambo mengine utayakuta kwenye kitabu🤣
Si kila jambo lazima nikwambie mengine tafuta kitabu hiki cha tajiri wa babeli usome mwenyewe.


Kumbuka no free lunch in America🤣🤣, ili kupata kitabu hiki utachangia kiasi cha Tsh 3,500 tu.

Kitabu kipo kwa lugha ya kiswahili na kingereza.

Imeandikwa na Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments