Moja ya kanuni muhimu katika maisha ya mafanikio ni kwamba kila mmoja wetu ili aweze kufikia kilele cha mafanikio yake ni kwamba ni lazima awe na afya njema. Kama mtu hautakuwa na afya njema ni kwamba utashindwa kuwajibika vyema kwenye maeneno muhimu unayofanya kazi.
Na siri pekee ambayo itakusaidia kuwa na afya njema na kuepeka na baadhi ya magonjwa ni kufanya mazoezi. Ni muhimu sana kufanya mazoezi angalau kwa dakika 20 kila siku, kwa sababu mazoezi ni tiba mbadala wa kuweka afya zetu katika hali nzuri saidi.
Lakini pia ni muhimu kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi humsaidia mtu ajisikie vizuri kabla ya kuanza na shughuli nyinginezo zinazomkabili kwa siku husika. Pamoja na hayo ni muhimu kufanya mazoezi ya mwili kwa sababu unapofanya mazoezi hata akili yako inachanagamka pia, wakati mwingine husaidia pia kuongeza uwezo wako wa kufikiri.
Ni muhimu kila mmoja wetu kuyafanya mazoezi mbalimbali ya mwili kila siku kwa sababu kuna faida lukuki zitokanazo na mazoezi. Mazoezi ni afya pia mazoezi ni muhimu kwa kila mmoja wetu. Anza sasa kuanza kufanya mazoezi kwani mazoezi ni muhimu sana.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments