Kama kuna jambo ambalo linatakiwa kufanyika, ni bora likafanyika mara moja, ukichelewa kulifanya unaweza ukajikuta una ahirisha na huwezi tena kulifanya jambo hilo.
Je, unawezaje kushinda kuahirisha mambo yako?
Hilo utaweza ikiwa kwanza utaangalia madhara yanayotokana na wewe kuahirisha mambo. Angalia jinsi utakavyozidi kukosa pesa kwa sababu umeahirisha kufanya mradi wako.
Angalia pia ikitokea kama hujaahirisha ni faida zipi utazipata? Najua utajifunza, utapata pesa na faida nyingine utazipata kwa sababu umefanya jambo hilo na umepambana.
Inawezekana kweli unaweza usiwe kamili na rasilimali kazi hazijatimia, lakini jitahidi tu kuchukua hatua na kamwe hata kidogo usije ukaahirisha jambo lako hata mara moja.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments