BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi umaskini unavyotengezwa.

Chukua hii,  Mara nyingi  umaskini wa mtu binafsi  huwa hautokani na kipato kidogo cha mtu huyo,  bali hutokana na jinsi mtu huyo anavyotumia zaidi ya kipato hicho.

Watu wengi pamoja na udogo wa vipato vyetu lakini matumizi yetu yamekuwa ni makubwa zaidi ya kile tunachopata. Kama unapata shilingi 100 basi matumizi yako yatakuwa ni shilingi 200,  yaani upo tayari kukopa ili kukidhi hata vitu visivyo vya msingi.

Wakati mwingine kitendo hiki cha kutumia zaidi ya vipato vyetu tulivyonavyo ndivyo vinavyotufanya tuendelee kuwa maskini kila siku na kila wakati. Hivyo ikiwa unataka kufikia kilele cha mafanikio yako epuka sana kutumia pesa zaidi ya kipato chako.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments