BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo Haya Mawili Ni Lazima Kwako, Ikiwa UTAWEKEZA.

Kama umefanya uwekezaji wowote ule, uwe uwekezaji kwenye hisa, biashara, kilimo au mahusiano, ni lazima utakuwa makini na kujitoa kwenye uwekezaji huo.

Kama kweli unatumia muda, pesa, na nguvu zako kwenye kitu hicho ulichowekeza, kaa ukijua kabisa, ni lazima utaweka umakini wako na kujituma kwa juhudi sana kwenye kitu hicho.

Kama unaona kujitoa kwako kuna lega lega kwa namna fulani hivi, unatakiwa kuwekeza. Unapokuwa umewekeza, umakini na kujitoa kunakuja kwenyewe tu. Wekeza leo uone.

Kama hujitoi kikamilifu, basi inawezekana hujawekeza. Wanaowekeza wanajitoa kuhakikisha mambo yao yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa na pasipo kukwama.

Weka akilini hii, ukiwekeza kwa kitu chochote kile,  UTAJITOA haswa kukamilisha lengo lako, kama usipowekeza kaa ukijua hutaweza pia kujitoa ili kufanikisha malengo yako.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.

 

Post a Comment

0 Comments