Kujiamini katika jambo lolote unalofanya kunatokana na mambo mawili, hatua unazochukua na changamoto unazokutana nazo. Hayo ndio mambo mawili yanaweza kukupa kujiamini na kutokuogopa.
Unapokuwa unajiamini, unaweza kufanya jambo lolote. Lakini, unatakiwa ujue, kujiamini huko kuna kuja kwa sababu ya jinsi unavyokubalina na changamoto zako na jinsi unavyochukua hatua zako kila siku.
Kama ambavyo misuli inajengwa, halikadhalika pia kujiamini kwako kunajengwa hivyo hivyo, siku hadi siku. Unavyoendelea kuchukua hatua na kushinda changamoto, unashangaa unajiamini sana.
Acha kukimbia au kuogopa changamoto, hizo zinakufundisha nidhamu, ushujaa, ujasiri na kujiamini. Changamoto yoyote ruksa kuja kwako, ikitoka inakupa fundisho kubwa sana kwako na la maana.
KITU CHA KUZINGATIA NA KUFANYA, weka akilini kwamba, kila siku unatakiwa kuchukua hatua juu ya ndoto zako, kwani kujiamini kwako kunatokana na unavyochukua hatua na kushinda changamoto, ni hivyo tu.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments