BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kama Hutaki Kufanya Kitu Hiki, Sahau Kupata Mafanikio.

Watu wengi hawataki kufanya kazi kubwa, ila wanataka mafanikio. Ni watu ambao kila wakati wanatafuta mafanikio makubwa, lakini hawataki kuweka kazi kubwa ya kuwapa mafanikio hayo.

Hiyo inakuwa ni sawa na mtu ambae anataka kuvuna na hajapanda kitu. Kama utaka mafanikio makubwa lakini wakati unachokifanya ili kupata mafanikio hayo hakionekani, unajidanganya wewe.

Ili kupata mafanikio makubwa unayoyataka, weka kazi sawa sawa na mafanikio unayoyataka. Ukiweka kazi sawa sawa na mafanikio unayoyataka uwe na uhakika utaweza kufanikiwa. Weka kazi, mafanikio utayapata.

Hakikisha kila wakati mafanikio yako, yaendane sambamba na kazi unayoweka. Kama itakuwa kinyume cha hapo nakwambia utakuwa unajidanganya sana. Amua kuweka kazi na utapata mafanikio makubwa  pia.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Post a Comment

0 Comments