Wafanyabiashara wowote wale waliofanikiwa kwenye dunia hii huwa wanao umoja unaofanana ambao huwa unawasaidia sana kwenye biashara wanazozifanya na hatimaye hupata mauzo na faida zaidi katika biashara zao.
Ikiwa wewe ni miongoni mwa wafanyabiashara hao kila wakati unapaswa ujifunze kuwa na mahusiano bora na wafanyabiashara wanzako hususani wale mnauza bidhaa zinazofanana.
Ukifanya hivyo ni lazima biashara zenu zitakuwa tu kwa sababu mtakuwa na tabia za ushirikiano baina yenu hususani sauala la kupeana wateja kwenye bidhaa ambazo mmoja wetu anakuwa hana au kaishiwa bidhaa hiyo.
Kuwa na ushirikiano baina yenu ni njia nzuri sana pia huongeza mauzo ya biashara kwa kiwango kikubwa. Mteja anapokuja dukani kwako kuhitaji huduma fulani kisha huduma hiyo au biashara hiyo ukawa huna usimwambie kuwa huduma hiyo huna, bali mwambie huduma au bidhaa hiyo ipo ngoja ukamchukulie stoo.
Huenda kweli hata hiyo stoo yenyewe ukawa huna na hiyo bidhaa ukaaa huna pia, unachotakiwa kufanya ni mwambie mteja huyo akusubirie kisha wewe nenda kwa majirani zako ambao mnaouza bidhaa zinazofanana kisha kamchukulie kile unachokihitaji umletee.
Kufanya hivi kutamfanya mteja huyo aje tena siku nyingine kununua kitu hicho kwa sababu ataamini kitu kile alikipata kwako hivyo hata siku nyingine unapokuwa anakihitaji kitu hicho atakuja moja kwa moja kwako.
Unapomwambia mteja kitu fulani huna, mteja huyo mara nyingi ataamini huenda hata siku nyingine akiwa anakihitaji kitu hicho ukawa huna tena. Hivyo jenga mahusiano bora na wafanyabiashara wenzako ili muweze kupata wateja zaidi kwenye biashara zenu.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments